Umuhimu wa Ngano katika Jamii ya Wasukuma: Uchanganuzi wa Kijamii na Kitamaduni

https://doi.org/10.58721/jkal.v4i1.1549

Authors

Keywords:

Kisukuma, Ngano, Urithi, Utamaduni

Abstract

Makala hii ni sehemu ya utafiti uliofanyika kabla katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Ililenga kubainisha umuhimu wa ngano katika jamii ya Wasukuma wa Kahama, Mkoa wa Shinyanga, kwa muktadha wa kijamii na kitamaduni. Utafiti ulifanyika katika vijiji vya Mpera, Iyenze, Isagehe na mtaa wa Nyakato, ukihusisha wazee 64 wenye umri wa zaidi ya miaka 70 waliopatikana kwa kutumia usampulishaji lengwa. Data zilikusanywa kupitia dodoso na mahojiano, ambapo zilichambuliwa kwa kutumia programu za SPSS kwa data za kitakwimu au za kiidadi, na ATLAS.ti kwa data za kimaelezo. Matokeo yalionesha kuwa washiriki wengi walikuwa na uelewa mkubwa kuhusu maana, umuhimu na matumizi ya ngano kama chombo cha kuimarisha maadili, mshikamano na kuhifadhi historia ya jamii. Wengine walitambua ngano kama visasili na visakale vinavyoeleza chimbuko la jamii, asili ya watu wake, na misingi ya mila na desturi zao. Aidha, utafiti huu umebainisha kwamba ngano ni urithi hai wa kitamaduni unaoendeleza utambulisho, maadili, na mshikamano wa jamii ya Wasukuma, sambamba na kutoa burudani na elimu kwa vizazi vinavyofuata. Utafiti unahitimisha kuwa ili kuhakikisha uendelevu wa urithi huu, ni muhimu kuweka mikakati ya kijamii na kielimu itakayohamasisha usimulizi wa ngano kwa vizazi vipya kupitia shule, makumbusho, na matamasha ya kitamaduni. Hatua hii itasaidia kuhifadhi na kuendeleza ngano za Kisukuma, na hivyo kuimarisha utambulisho na urithi wa kitamaduni wa Kiafrika.

Published

2026-02-05

How to Cite

Balele, J. M., & Msonde, S. E. (2026). Umuhimu wa Ngano katika Jamii ya Wasukuma: Uchanganuzi wa Kijamii na Kitamaduni. Journal of Kiswahili and Other African Languages, 4(1), 1–12. https://doi.org/10.58721/jkal.v4i1.1549

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.